Molekuli Quotes

Quotes tagged as "molekuli" Showing 1-2 of 2
Enock Maregesi
“Watoto hupenda vitu vinavyong’aa ambavyo havijatulia na vilivyopangiliwa vizuri. Hivyo ndivyo macho ya binadamu yalivyo: yana unyevu na yanaakisi mwanga, hayajatulia, na yana rangi kadha wa kadha ikiwa ni pamoja na kope na vigubiko vya macho ambavyo pia hazijatulia. Mtoto mchanga hasa yule anayeona vizuri huangalia macho pale anapopata nafasi, kwa maana ya kuyashangaa. Vilevile, huangalia macho kwa maana ya kupokea molekuli ya maadili au homoni inayorahisisha maisha kutoka kwa mama yake iitwayo ‘oxytocin’. ‘Oxytocin’ husisimua ubongo wake na kuutayarisha kupokea neno lolote litakalosemwa na mama yake mzazi au mama yake mlezi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kila binadamu ana nguvu ya ziada katika mwili wake ijulikanayo kitaalamu kama ATP. ATP (‘Adenosine Triphosphate’) ni molekuli ndogo zaidi iliyoko ndani ya seli ambayo kazi yake ni kutengeneza nguvu ya ziada kwa ajili ya seli, na kwa ajili ya mwili mzima kwa jumla, pale mwili unapoonekana kukata tamaa au kuishiwa na nguvu kabisa. Ni kama jenereta ya umeme kwa ajili ya seli, inayofanya kazi pale umeme wa kawaida unapokatika.”
Enock Maregesi